BURUNDI WATUA BONGO, KUIVAA STARS JUMANNE HII - CAPITAL TZ BLOG DODOMA

Latest

BANNER 728X90

Sunday, 26 March 2017

BURUNDI WATUA BONGO, KUIVAA STARS JUMANNE HII


Intamba Mu Rugamba timu ya taifa ya Burundi imewasili leo  ikitokea Bujumbura kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Tanzania utakaopigwa Jumanne ya March 28.

Timu hiyo imewasili ikiwa na baadhi ya wachezaji wao muhimu akiwemo Laudit Mavugo ambapo Mchezo huo upo katika kalenda ya shirikisho la soka duniani FIFA utafanyika katika uwanja wa taifa Dar es Salaam .

Aidha huo utakuwa mchezo wa pili wa kirafiki kwa Taifa Stars ilishinda bao 2-0 dhidi ya Botswana.