Nay wa Mitego afikishwa Central Polisi DSM, Wakili Peter Kibatala kayaandika haya - CAPITAL TZ BLOG DODOMA

Latest

BANNER 728X90

Sunday, 26 March 2017

Nay wa Mitego afikishwa Central Polisi DSM, Wakili Peter Kibatala kayaandika haya

Baada ya jeshi la Polisi mkoan Morogoro kuthibitisha kukamatwa kwa msanii wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego sasa basi taarifa  iliyonifikia ni kwamba tayari ameshafikishwa Kituo cha Polisi Kati Dar es salaam jioni hii.
Sasa miongoni mwa wakili walioguswa kwa kukamatwa kwa msanii huyo ni wakili Peter Kibatala ambae kupitia ukurasa wake wa instagram aliyaandika haya….>>>Nay wa Mitego amefikishwa Central Police Station, Dar es Salaam yuko salama na imara amekula pia. Kwa kuwa amefika jioni sana; hakuna kinachoweza kufanyika leo Wakili Faraji Mangula alifika pale, na kesho tutapigana afikishwe Mahakamani au apewe dhamana‘- Peter Kibatala
ULIIKOSA HII YA POLISI MOROGORO KUHUSU KUMKAMATA NAY WA MITEGO BASI BONYEZA PLAY KUMSIKILIZA KAMANDA WA POLISI  MATEI KWA UFAFANUZI ZAID