
Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Mbwana Samatta ameaomba watanzania kujitokeza kwa wingi kuipa support timu hiyo itakaposhuka uwanjani kesho kuivaa Botswana ili iweze kufanya vizuri.
Akizungumza leo hii mchezaji huyo amesema kuwa licha ya ugeni wa timu ya Botswana bado anayo imani kwa timu ya Tanzania kufanya vizuri katika mchezo huo ikichagizwa na uwezo wa vijana waliopo kikosini.
Aidha Samatta amedai kuwa mchezo huo utakuwa ni kujipima nguvu na itampa fursa kocha mkuu wa timu hiyo Salum Mayanga kukipanga vyema kwa mashindano kikosi chake.
Zaidi msikilize hapa nahodha huyo