BRAZIL YASHINDA 4-1 UGENINI, ARGENTINA NAO WATAMBA NYUMBANI - CAPITAL TZ BLOG DODOMA

Latest

BANNER 728X90

Thursday, 23 March 2017

BRAZIL YASHINDA 4-1 UGENINI, ARGENTINA NAO WATAMBA NYUMBANI


Michuano ya kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi imeendelea kutimua vumbi usiku wa kuamkia leo katika bara la America ya Kusini.

Brazil imeifunga Uruguay bao 4-1 ,magoli ya Paulinho 18',52' 90' na Neymar 75' huku bao la kufutia machozi la Uruguay likifungwa mapema dk ya 8 kwa mkwaju wa penalt kupitia kwa Edison Cavan.

Nao Argentina wameshinda 1-0 dhidi ya Chile bao pekee likigungwa na Lionel Messi kwa mkwaju wa penalt dk ya 16, Paraguay wao walishinda 2-1 dhidi ya Ecudor na Venezuela walitoka 2-2 dhidi ya Peru.

Hata hivyo matokeo hayo yametengeneza mazingira mazuri kwa Brazil kutinga kwenye fainali hizo ambapo sasa wana alama 30 wakifuatiwa na Uruguay wenye alama 23 nafasi ya tatu ni Argentina alama 22.