Emanuel Martin Joseph alizidi kupata umaarufu mkubwa katika mchezo wa kirafiki uliochezwa Disemba 10 Yanga ikifungwa 2-0 uwanja wa uhuru
Klabu ya Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar (JKU) imethibitisha kumalizana kila kitu na klabu ya Yanga kwa Mshambuliaji wao Emanuel Martin Joseph.
Katibu mkuu wa Klabu ya JKU Sadu Ujudi amethibitisha taarifa hizo kwa kusema kuwa tayari JKU na Yanga wameshamalizana kila kitu kuhusu mchezaji huyo kujiunga na Jangwani ambapo amesema kwasasa tayari mchezaj huyo yupo Yanga.
Emanuel Martin Joseph alizidi kupata umaarufu mkubwa katika mchezo wa kirafiki uliochezwa Disemba 10, 2016 katika uwanja wa Uhuru ambapo Yanga ilifungwa mabao 2-0 dhidi ya JKU ambapo mabao yote siku hiyo alifunga Martin.
Martin alifunga bao la kwanza dakika ya 12 kwa shuti kali akiunganisha kona iliyopigwa na Mbarouk Chande wakati la pili alifunga dakika ya 27 akimalizia pasi ya Nassor Mattar.