MABINGWA wa Ulaya Real Madrid wakiongozwa na Mchezaji Bora Duniani Cristiano Ronaldo Leo wametinga Fainali ya Mashindano ya FIFA ya Kombe la Dunia kwa Klabu huko Yokohama International Stadium Nchini Japan kwa kuwachapa Club America Bao 2-0.
Bao za Real, ambao sasa wamefikisha Mechi 36 mfululizo bila kufungwa, zilifungwa na Karim Benzema na Cristiano Ronaldo katika Dakika za 47, kipindi cha Kwanza, na 93.
Lakini Bao la Pili, ambalo alifunga Ronaldo, ilibidi lipasishwe na VARs, Msaada wa Teknolojia ya Video, ambalo liliangaliwa kwenye Video pembezoni mwa Uwanja kama lilikuwa Ofsaidi au la.
Hatimae Bao hilo likakubaliwa.
Kwenye Fainali, hapo Jumapili, Real watavaana na Kashima Antlers ambayo ni Klabu Wenyeji kutoka Japan.
Ikiwa Real watatatwaa Taji hili basi litakuwa ni Kombe la Dunia lao la Pili katika Kipindi cha Miaka Mitatu.
++++++++++++++++++++++++++++++
Sikiliza hapa uchambuzi wa mechi hiyo na Abbas Pira