UCHAMBUZI (AUDIO)-UEFA CHAMPIONS LEAGUE, CELTIC KUICHAPA CITY? ARSENAL JE ? TUSUA MKEKA HAPA - CAPITAL TZ BLOG DODOMA

Latest

BANNER 728X90

Tuesday, 6 December 2016

UCHAMBUZI (AUDIO)-UEFA CHAMPIONS LEAGUE, CELTIC KUICHAPA CITY? ARSENAL JE ? TUSUA MKEKA HAPA

UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, Hatua ya Makundi, inafikia tamati Leo Jumanne kwa Makundi A hadi D na baadhi ya Makundi yake Timu zilizofuzu tayari zimepatikana na kilichobaki ni kuamua nani Mshindi wa Kundi.
Tayari Timu 12 zimeshafuzu Hatua ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 na kubakisha Timu 7 kugombea Nafasi 4 zilizobaki.
Kundi A, Arsenal na Paris Saint-Germain, zimeshasonga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 na kilichobaki kuamua ni nani Mshindi wa Kundi na pia Timu ipi inamaliza Nafasi ya 3 ili iende kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI Raundi ya Mtoano ya Timu 32.
Kwa Kundi B, vita ya kufuzu ipo kwa Timu 3, Napoli, Benfica na Besiktas, wakati Dynamo Kiev imeshatupwa nje kabis.
Kwa Kundi C, kazi imekwisha baada ya Barcelona kutwaa ushindi wa Kundi, Man City kuchukua Nafasi ya Pili na Borussia Monchengladbach kutupwa Nafasi ya 3 na hivyo kupelekwa EUROPA LIGI.
Kwenye Kundi D, Atletico Madrid wametwaa ushindi wa Kundi na Bayern Munich Nafasi ya Pili.
Rostov na PSV Eindhoven watagombea nani kucheza EUROPA LIGI.

RATIBA Jumanne 6 Desemba 2016
KUNDI A
FC Basel v Arsenal
Paris Saint Germain v Ludogorets Razgrad                 
KUNDI B
Benfica v Napoli               
Dynamo Kiev v Besiktas             
KUNDI C
Barcelona v Borussia Monchengladbach           
Manchester City v Celtic
KUNDI D
Bayern Munich v Atlético Madrid           
PSV Eindhoven v FC Rostov        
+++++++++++++++++++++++++++++++++
Sikiliza hapa uchambuzi wa mechi ya man city vs celtic