Shirikisho la soka nchini TFF limeahidi kusambaza ratiba ya mzunguuko wa pili wa ligi kuu ya soka Tanzania bara kwa klabu 16 za ligi hiyo ndani ya juma hili.
Afisa habari wa TFF Alfred Lucas amesema tayari taratibu za maandalizi ya ratiba ya mzunguko wa pili zimeshakamilika na wanaamini kila jambo lililopangwa kweye ratiba hiyo liutakamilishwa kwa wakati.
Hata hivyo Alfred amesema upangaji wa ratiba ya mzunguuko wa pili wa ligi kuu, umezingatia ratiba za michezo ya shirikisho la soka duniani FIFA ambazo kwa sasa zinazingatia michezo ya kuwani kufuzu fainali za kombe la dunia.