Baada ya kusubiri kwa muda mrefu. Hatimaye Zari The Bosslady na Diamond wamefanikiwa kuongeza familia mpya kwa Mtoto huyo wa kiume kuzaliwa saa 10 na 35 Alfajiri kwa saa za Afrika Mashariki, Jumanne, December 6.
Mtoto huyo amezaliwa kwenye hospitali ya NETCARE ya Pretoria nchini Afrika Kusini. Tayari Diamond na Zari wameonesha picha za mtoto huyo japo hawajaweka sura yake na bado hawajasema wamemwita jina gani.