EPL, Ligi Kuu England, inaendelea tena Leo kwa Mechi 3 lakini Bigi Mechi ni huko Etihad Jijini Manchester wakati Wenyeji Manchester City wakiivaa Arsenal.
Kwa sasa EPL inaongozwa na Chelsea, ambao Jana waliifunga Crystal Palace 1-0, na kuwa Pointi 9 mbele ya Timu za Liverpool na Arsenal zinazofungana kwa Pointi zote zikiwa na Pointi 34 kila mmoja ila Liverpool wapo juu kwa Ubora wa Magoli.
Timu ya 4 ni Man City ambao wako Pointi 1 nyuma ya hizo Timu 2 zikifuata Tottenham na Man United zote zikiwa na Pointi 30 kila mmoja.
Wakati, City na Arsenal zikipambana Leo, Liverpool wao wanacheza Jumatatu Usiku huko Goodison Park dhidi ya Mahasimu wao wakubwa Everton katika Dabi ya Merseyside.
Michezo mingine leo Bournemouth watacheza na Southampton naTottenham Hotspur itakuwa nyumbani kwao White Hart Lane kuivaa Burnley
The Capitaltz.com tunakuunganisha na Abbas Pira moja ya watanzania waishio nchini Uingereza na kuwahi kufanya majaribio katika vilabu vikubwa nchini humo zikiwemo Chelsea Fc, Mk Dons, Birmigham City, Colchester United hapa anauchambua mchezo wa Man City dhidi ya Arsenal.