MWILI WA ISMAIL KUZIKWA LEO MWANZA - CAPITAL TZ BLOG DODOMA

Latest

BANNER 728X90

Monday, 5 December 2016

MWILI WA ISMAIL KUZIKWA LEO MWANZA

Katika tukio la kusikitisha lililotokea jana Mshambuliaji wa klabu ya soka ya Mbao Fc u20 Ismail Khalfan Mrisho alikutwa na umauti katika hali ya kusikitisha sana. Katika mchezo wa jana uliozikutanisha Mbao fc na Mwadui Fc katika ligi ya vijana chini ya umri wa miaka 20.
Ismail aliipatia Mbao fc bao safi la kuongoza kwa kisigino na kushangilia kwa staili ya aina yake punde baadae alikwaana na mchezaji mwenzake tukio ambalo lilimfanya Ismail ashindwe kuinuka.
Aidha makamu Mwenyekiti wa klabu ya Mbao Fc Erick Goso alisema walikuwa wanafuatilia taratibu za kitabibu ili waweze kupewa mwili na wamelikamilisha hilo tayari na sasa kitu pekee ni kuupeleka mwili kwao Mwanza ili taratibu za mazishi zifuatwe.
“Kutokana kuwa Mchezaji wetu ni muumini wa dini ya kiislamu na familia imetoa tamko kwamba azikwe leo jioni na endapo mwili utachelewa sana basi atazikwa kesho mapema ingawa hatutarajii hilo”.
The Capital Tz.Com  inaungana na wadau wote wa familia ya mpira katika kuomboleza kifo cha mchezaji huyo chipukizi. Hakika kazi yake mola haina makosa.