AUDIO-SIMBA WAWEKA TUMAINI KWA AGYEI, MANARA AFUNGUKA KWA WADAU WA SIMBA KUVUTA SUBRA - CAPITAL TZ BLOG DODOMA

Latest

BANNER 728X90

Monday, 5 December 2016

AUDIO-SIMBA WAWEKA TUMAINI KWA AGYEI, MANARA AFUNGUKA KWA WADAU WA SIMBA KUVUTA SUBRA


Vinara wa ligi kuu ya soka Tanzania bara Wekundu wa Msimbazi Simba wamejinasibu kuwa na matumaini makubwa na mlinda mlango wao mpya kutoka nchini Ghana Daniel Agyei ambae wamemsajili kupitia dirisha dogo litakalofungwa rasmi Disemba 15.

Afisa habari wa klabu ya Simba Haji Manara amesema kipa huyo ambae amemalizana na klabu ya Medeama kimkataba atakua tegemeo na nguzo kuu kwenye harakati zao za kuwani ubingwa kwa msimu huu wa 2016/17.

Amesema wanaamini ujio wa Agyei utaleta chachu ya kuwani nafasi ya kukaa langoni kwa makipa wengine waliopo kikosini Vicent Agban pamoja na Manyika Jr.

Manara pia amezungumzia sababu ambazo ziliufanya uongozi wa klabu ya Simba kumuangalia kwa jicho la tatu mlinda mlango huyo kutoka nchini Ghana ambaye aliwahi kuja nchini akiwa na kikosi cha Mediama kilichocheza na Young Africans kwenye michuano ya kombe la shirikisho.

Mbali na kutoa sababu za kusajiliwa kwa kipa huyo, Manara amewasisitiza wanachama na mashabiki wa Simba kuwa na subra ya kuona wachezaji wengine wakisajiliwa kabla ya dirisha dogo kufungwa Disemba 15.