Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu imeeleza kuwa Minja anastaafu kuanzia leo tarehe 02 Desemba, 2016.
Rais Magufuli amempongeza Kamishna Jenerali wa Magereza Mstaafu John Casmir Minja kwa utumishi wake na amemtakia maisha mema ya kustaafu.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Kamishna wa Magereza (CP) Dkt. Juma A. Malewa kuwa Kaimu Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini hadi hapo uteuzi wa Kamishna Jenerali wa Magereza utakapofanyika.
Rais Magufuli akiwa na John Minja Nov 29 mwaka huu alipofanya ziara ya kushtukiza katika magereza ya Ukonga DSM.
Novemba 29 mwaka huu, Rais Magufuli alifanya ziara ya kushtukiza katika magereza ya Ukonga Dar es Salaam na kutoa maagizo kadhaa ikiwemo kupiga marufuku sare za majeshi kuuzwa na watu binafsi.
Kadhalika Rais Magufuli alipiga marufuku kwa majeshi yote nchini kuingia ubia na watu binafsi kupangisha ama kuuza maeneo yao kwa ajili ya kufanya biashara na kutaka maeneo yote ya majeshi yabaki katika jeshi husika.