Tunafahamu kwamba Rais Magufuli alitangaza kuwa ndani ya miaka minne serikali yake yote itakuwa imehamia Dodoma, juzi pia tukasikia mkakati wa serikali kuifanya Dodoma kuwa jiji. Leo Mkurugenzi wa manispaa Godwin Kunambi amekutana na waandishi wa habari na kuelezea mipango mikakati ya kuhakikisha Dodoma inakwenda kuwa makao makuu..
‘Manispaa ya Dodoma tumejipanga vizuri, unapozungumzia uwekezaji wowote lazima utazungumzia miundombinu kama vile barabara, maji, elimu, shule, afya n.k‘ –Godwin Kunambi
‘Juzi tumepitisha Dodoma kuwa jiji na katika hili ni lazima tujipange vizuri, tumejipanga kukuboresha barabara zote za kuzunguka mji wetu pia tunakwenda kujenga stend kubwa ya kisasa maeneo ya nanenane na tupo katika mkakati wa mwisho‘ –Godwin Kunambi
‘Tumepanga kuwa na soko kuu la kisasa ikiwa ni pamoja na kuboresha lile la sabasaba, katika bajeti ya 2017/2018 tunakwenda kuboresha huduma za kiafya ikiwa ni pamoja na kuifanya hospitali ya Makole kuwa hospitali ya kisasa katika ngazi ya Wilaya‘ –Godwin Kunambi
‘Kuhusu suala la viwanja watu wasiwe na hofu viwanja vinapatikana vya kutosha, mchakato uliopo sasa ni kuendeleza masuala ya vipimo kutoka kwa ndugu zetu CDA‘ –Godwin Kunambi
Unaweza kuendelea kumsikiliza mkurugenzi wa jiji kwenye hii video hapa chini…..
ULIIKOSA HII SIMULIZI YA MWANAFUNZI ALIYEBAKWA NA KUPEWA MIMBA NA MWALIMU