Ikiwa bado taarifa ya Young D kupata mtoto ikiendelea wakihoji na kujipa maswali juu ya mahusiano ya rapper huyo na mpenzi wake Tunda,mengine mengi yanaendelea kuibuka.
Story inazidi kua kubwa pale Amber Lulu,video vixen aliekua mpenzi wa Young D kujitokeza hadharani na kuthibitisha atamlea mtoto wa Young D kama mwanae,Amber Lulu kadai kua atakua mama bora kwa mtoto huyo,ambaye yeye anamuita mama mdogo.
"Tammy wetu 😍😍💪💪💪💪Nakulea mwenywe mom nakupromise ntakuwa mom mdogo bora kabsaa watashangaa" aliandika Amber katika kurasa yake ya instagram
Mpaka sasa Tunda hajatoa tamko lolote juu ya kinachoendelea mitandaoni ukizingatia ndio kwanza wametoka kurudia juzi juzi.
Story za kuwepo kwa mahusiano kati ya Amber na Young D ziliwahi kuvuma ingawa wawili hao wanasema walikua marafiki tu ingawa walikua wakishiriki mapenzi.