bongo movies tumepata pigo baada ya mwigizaji mwenzetu Jaji Khamis ( kashi) alifariki dunia katika hospitali ya muhumbili alipokuwa amelazwa. Msiba huu unakuwa ni mwendelezo wa majanga na misiba inayowakumba wasanii na watu maafuru nchini ikiwa ni siku chache tuu zimepita toka tulipomzika msanii wa muziki wa kizazi kipya Albert Mangwea aliyefariki huko Afrika ya kusini kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni utumiaji mkubwa wa dawa za kulevya.
Tukiwa bado kwenye wiki hii ya msiba tumeweza kupata comments za mastaa tofauti wa tasnia ya uigizaji waliyosema jana baada ya taarifa za msiba wa kashi kuwafikia. Ila jambo ambalo limeonekana kuwatatiza wote jana ni “kwanini maisha ya wasanii yanakatika hivi”? Why? Ni Swali gumu na ambalo wengi wetu hatuwezi kuwa na jibu moja la uhakika maana Mungu ndo ajuaye yote na muweza yote. Apangalo Maanani hamna anayeweza kulipangua. Cha msingi ni kukaa katika njia zake yeye.
Thursday, 13 June 2013
New
About Unknown
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
