Dar. Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Seif Shaban maarufu
kama Matonya bado anaendelea kusota rumande mjini Songea baada ya
kukataliwa dhamana kutokana na kufanya utapeli baada ya kulewa kupita
kiasi na kushindwa kufanya shoo iliyoandaliwa na promota mmoja mjini
humo.
Matonya alitakiwa kufanya shoo kwenye Ukumbi wa Jambolee uliyopo Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
Matonya alifika ukumbini akiwa amelewa hali
iliyompelekea kushindwa kufanya show na kusababisha hasara katika ukumbi
baada ya kufanya fujo ya kuvunja vitu ukumbi hapo, Ndipo waandaaji wa
show hiyo walipoamua ifanyike kesho yake na kiingilio kiwe ni kununua
bia .
Wakati huo msanii huyo alitakiwa akafanye show
nyingine Wilaya ya Mbinga ambayo ilikuwa ni sehemu ya mkataba wao lakini
hakufanya hivyo na matokeo yake akaamua kukata tiketi kurudi Dar es
Salaam. Baada ya kuvuja taarifa hizo walimfata hadi alipokuwa amefikia
na kukuta amehamia sehemu nyingine ..........(Mwananchi)
