MANENO MAZITO ALIOYATOA MSANII WA BONGO MOVIE -- Flora Mvungi (“Mniache na ndoa yangu,itadumu milele” .....ZAIDI “Mi na H-baba tunapendana”) - CAPITAL TZ BLOG DODOMA

Latest

BANNER 728X90

Thursday, 13 June 2013

MANENO MAZITO ALIOYATOA MSANII WA BONGO MOVIE -- Flora Mvungi (“Mniache na ndoa yangu,itadumu milele” .....ZAIDI “Mi na H-baba tunapendana”)

 
Msanii wa bongo movies Flora mvungi ambaye hivi majuzi alifunga ndoa ya kimya kimya na msanii mwingine kwenye upande wa bongo fleva amewataka watu wote walioanza kuichokonoa ndoa yake hiyo kwa kauli kuwa “itadumu mwaka mmoja tuu” wamuache kwa amani kwani itadumu milele kwakuwa yeye na H-baba wanapendana na wamekuwa wakichunguzana tabia kwa muda mrefu kabla ya kuamua kuoana.

Katika mahojiano aliyoyafanya na mwandishi wa mtandao wa global publishers Imelda Mtema, flora mvungi amesema yeye na mpenzi wake huyo walishakaa muda mrefu na kuchunguzana, hawakukurupuka kuingia kwenye ndoa hivyo siyo rahisi kuachana kwa midomo ya washakunaku kama walivyotabiri.
“Wanikome! Wanaongea tena… alimalizia Flora mvungi.