Katika kusikiliza wimbo mpya ya mwanadada LADY JAYDEE uliotoka hivi karibuni ukitambulika kwa jina YAHYA, nikaona kama ina ukweli fulani ndani yake na ndipo nilipoamua kumuuliza muhusika na kunijibu kuwa Yahya
ni wimbo alioutunga kutokana na tabia za baadhi ya watu tunaoishi nao
katika maisha yetu ya kila siku na maisha yao ni uongo wa kusabisha
utapeli kwa watu na mali zao akiwemo huyo YAHYA.
Katika pitapita na uchunguzi, GongaMx TEAM imegundua kuwa YAHYA yupo na anaendelea na mambo yake ya utapeli na uongo baada ya kufuma taarifa kwenye mtandao wa jamii wa Facebook iliyoandikwa na Mr. JOHN wa huko Arusha kuwa YAHYA aka HISBERT akimtambulisha kama “A New TAPELI IN ARUSHA” kuwa amefanikiwa kukutana na YAHYA na ameweza kuhadithia aliyokutana nayo baada ya kukutana nae.
