Watu wanne
wamefikishwa Mahakamani wakituhumiwa kutenda kosa la kufanya unyang’anyi wa
kutumia Silaha kwa kumpora Askari Magereza Bunduki na hukumu ikitolewa kwa
Mshtakiwa mmoja ambaye amehukumiwa miaka 30 jela.
Mwendesha Mashtaka wa
Serikali Mwajabu Tengeneza akisoma Mashtaka Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama
ya Wilaya ya Mbeya Aneth Nyenyema amesema Washtakiwa wote wanne kwa
pamoja walitenda kosa hilo kinyume cha Sheria ya kanuni ya adhabu kifungu cha
287(A) sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Amewataja watuhumiwa
kuwa ni Ali Salum (32) ambaye ni mshtakiwa namba moja akiwa na Emmanuel
Martin(25), Braison Sanga na John Waziri(22) ambao ilidaiwa kuwa Mei 5, Mwaka
katika eneo la Magereza Songwe walimvizia askari WDR Ambrose na kumjeruhi kisha
kumpokonya bunduki aina ya SRA yenye namba za usajili TZ PS 39847164020 mali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kitengo cha Jeshi la Magereza.
Kutokana na Mashtaka
hayo watuhumiwa wote walikana isipokuwa Mshtakiwa namba moja ambaye alikubali
kutenda kosa hilo hali iliyomlazimu Mwendesha mashtaka kumsomea mara tatu ili
kujua kama ameelewa mashtaka yake.
Na Mbeya yetu