“Hakuna chama cha siasa ambacho kina thamani sawa na uhai wa binadamu, mtu kuwa chama anachotaka hajafanya kosa hata kustahili kuuawa, kwa maana hiyo mimi kila nikitafakari naona kuna kamchezo kanakochezwa, hatutawaacha wanaoua na wala hatutawaacha wanaoshirikiana na wanaoua.”
Hiyo ni kauli ya Waziri wa Mambo ya ndani, Mwigulu Nchemba wakati alipotembelea katika eneo la Kibiti kwa mara nyingine na kuzungumza na Askari Polisi ambao wako kwenye Operesheni ya kuhakikisha wanakomesha matukio ya mauaji.
Hii ni kufuatia mauaji ya Mwenyekiti mstaafu wa CCM wilayani Kibiti Pwani ambaye aliuawa siku kadhaa zilizopita kwa kupigwa risasi akiwa nyumbani kwake, tukio hilo ni mfululizo wa matukio ya mauaji mkoani Pwani.