CHIN BEES AWANYONGA NYONGA, AJA NA AUDIO/ VIDEO - CAPITAL TZ BLOG DODOMA

Latest

BANNER 728X90

Monday, 22 May 2017

CHIN BEES AWANYONGA NYONGA, AJA NA AUDIO/ VIDEO



Baada ya kujitengenezea heshima adimu kama ‘Prince wa Trap’ Tanzania kupitia ngoma yake, Pepeta, Chin Bees ameachia wimbo mpya ‘Nyonga Nyonga’ pamoja na video yake.
Wimbo huo wenye mahadhi ya dancehall iliyochanganyikana na ladha za aina yake za Kibongo, unadhihirisha uwezo wa Chin katika kubadilika kwenye mahadhi mbalimbali kama atakavyo. Nyonga Nyonga ambao ni wimbo wa pili wa rapper huyo akiwa chini ya usimamizi wa label ya Wanene Entertainment.
Nyonga Nyonga imetayarishwa na Dk. Reggy, mpishi ambaye amewahi kufanya miradi mingi na Chin Bees siku za nyuma. “Dk. Reggy ni producer wangu wa kwanza kabisa, nimeanza kufanya naye kazi kitambo kabla hata sijawa na jina kubwa,” anafafanua.
Video ya wimbo huo imefanyika katika mitaa mbalimbali ya Dar es Salaam huku rangi za nguo walizovaa wote wanaoonekana, zikitengeneza picha ya kuvutia machoni na yenye Uafrika mwingi.
Kuhusiana na video hiyo Chin amesema, “imefanyika hapa hapa Wanene na tuliamua kuifanyia nje zaidi tofauti na video yangu iliyopita ya Pepeta ambayo yote ilifanyika ndani. Tumefanya kwenye yale mazingira ya mtaani kabisa.”