MASH JAY ASIKITISHWA NA MZIKI WA MOROGORO KUKOSA UMOJA - CAPITAL TZ BLOG DODOMA

Latest

BANNER 728X90

Tuesday, 18 April 2017

MASH JAY ASIKITISHWA NA MZIKI WA MOROGORO KUKOSA UMOJA

Mash Jay msanii wa muziki wa Hip Hop kutoka mkoani Morogoro amesikitishwa na nguvu ndogo ya support kutoka kwa wasanii wakubwa mkoani hapa ambao wametangulia katika mziki nchini Tanzania.

Akizungumza katika kipindi cha Ladha 3600 kinachoruka kupitia radio E Fm, Msanii huyo amesema kuwa licha ya wasanii wengi wachanga kutoka mkoani hapa kujitahidi kufanya kazi, bado kazi hizo ambazo wanazifanya kwa ubunifu mkubwa zinakosa ushirikiano hata kutoka kwa wasanii wakubwa wa Moro Town.

"Tunajaribu kufanya vitu tofauti, Moro ukweli hakuna umoja wa wasanii na huu ugonjwa umeanza tangu kipindi kina Afande Sele, Stamina yaani hawatoi ushirikiano kwa upcoming' alisema Mash Jay.

Hata hivyo Mash kwa sasa ameachia single mpya aliyofanya kwa producer Vent Skillz chini ya studio za kwanza records, wimbo huo unaitwa MR.Masumbuko.