Akizungumza na Capitaltz.com meneja wa Belle 9 Jahz Zamba amethibitisha taarifa hiyo kwa kusema “ni kweli baba yake Belle 9 amefariki nataraatibu ni mazishi kesho saa nane kwasababu
ameumia sana kwahiyo msiba hauwezi kukaa muda mrefu”Alisema.
"Amegongwa na Boda boda yaani boda boda ilikuwa inatoka speed ikaja
ikamgonga kwahiyo hata huyu dereva boda boda ameumia vibaya sana kabla ya kumpeleka
hospitali ambako mauti yalimkuta…timu nzima ya vitamini music wameondoka na
Belle 9 kwahiyo wapo kwenye kushughulikia masuala yote ili kuwa bega kwa bega
na mwenzetu” Alisema Jaz.
Kwa niaba
ya timu nzima ya Capitaltz.com tunatuma salamu za pole kwa ndugu jamaa na
marafaiki walioguswa na msiba huo.