Mabao ya Philipe Coutinho,Neymar na Marcelo yametosha kuipa ushindi wa mabao 3-0 timu ya taifa ya Brazil katika mchezo dhidi ya Paraguay kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia 2018 nchini Urusi.
Brazil wakiwa nyumbani kwao katika mchezo uliofanyika alfajiri ya leo imeendeleza wimbi la kutopoteza kwa mchezo wa 8 mfululizo chini ya kocha Tite ambapo sasa wametimiza alama 33 na kujiongezea nafasi ya kuwa timu ya kwanza kufuzu fainali hizo.
Nao Argentina wakicheza ugenini bila staa wao Lionel Messi alikitumikia kifungo cha kukosa mechi 4 walifungwa 2-0 na Bolivia.
Matokeo mengine Ecuador walifungwa 2-0 nymbani kwao dhidi ya Colombia nao Chile waliifunga Venezuela 3-0.

