WAKILI Albert Msando Akatwa Katwa Mapanga Dar - CAPITAL TZ BLOG DODOMA

Latest

BANNER 728X90

Monday, 19 December 2016

WAKILI Albert Msando Akatwa Katwa Mapanga Dar



Ndugu zangu, nawashukuruni wote mliojaribu kunitafuta na kunipa pole toka jana. Sikuwa napatikana kwa sababu walionivamia waliiba simu pamoja na vitu vingine.

Kilichotokea: Usiku wa saa tano siku ya Alhamisi (juzi) nilisimamishwa na gari baada kupigiwa honi na kuwashiwa taa na gari iliyokuwa nyuma yangu. Niliposhusha kioo driver akawa anaongea haraka haraka kwamba nimewagonga wakati narudi nyuma parking na nakimbia. Nikamjibu kwamba sijamgonga.

Akaniambia umetugonga angalia bampa. Kweli bampa lilikuwa limelegea. Ila sikuwa nimewagonga hivyo nikaendelea kubisha. Akaniambia shuka uangalie hata pembeni. Alikuwa amevaa smart tu so nikashuka. Wakati naangalia anaposema nimemgonga wakashuka wengine wawili kutoka kwenye gari na kunishika. Wakaanza kunishambulia huku wakinipora wallet, saa nk. Then wakanikata panga kichwani na kupekua gari wakaondoka na laptop na simu pamoja na funguo wa gari.

Kwa sasa naendelea vizuri baada ya kupata matibabu. Nawashukuru wote.

Albert Msando