HAZARD NA JAMES RODRIGUEZ KUPISHANA
Miamba ya soka ya Hispania Real Madrid ipo katika mipango ya kumzuia James Rodriguez asiondoke mwezi Januari ili waweze kumtumia katika dili la kumvuta Eden Hazard na golikipa Thibaut Courtois.
Chelsea ambao wanajiandaa kutoa dau la paundi milioni 63 ili kumpata kiungo mshambuliaji huyo watapata wakati mgumu kwani Madrid inamuhitaji Hazard ambaye ni tegemezi ndani ya vijana hao wa Antonio Conte.
Kutokana na kila upande kutaka mchezaji kwa mwenzake hivyo inasemekana kufanya dili ya kubadilishana wachezaji litakalowahusu Rodriguez, Courtois na Hazard.
SEVILLA WAMTAKA MARTIAL
Mshambuliaji wa Manchester United Antonio Martial huenda akajiunga na Sevilla mwezi Januari baada ya klabu hiyo kuonesha nia ya kutaka kumsajili.
Gazeti la Express la Uingereza limetaarifu kuwa Sevilla wapo tayari kumchukua Martial kwa mkopo wa miezi 6 katika dirisha dogo la usajili mwezi Januari.
Martial angependa kupata nafasi zaidi ya kucheza kwani chini ya kocha Jose Mourinho nafasi yake imepungua zaidi dimbani.
Sevilla wanafikiria kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji ili kujihakikishia nafasi za juu zaidi katika ligi kuu nchini Hispania huku wawakilishi wa Martial wakiwa wamefanya mazungumzo na viongozi wa klabu hiyo mwezi uliopita.
BACCA KUBAKIA MILAN
Mshambuliaji wa AC Milan Carlos Bacca ambaye amekuwa akihusishwa na kujiunga na klabu mbalimbali barani Ulaya ameamua kubaki kwa miamba hiyo ya Italia.
Suso Fernandez ambae anacheza nae Milan alisema “nafikiri hivyo nilimuuliza Bacca ukaniambia ana furaha klabuni hapa na najua atabakia hapa ila katika soka kila kitu hubadilika kulingana na nyakati ila itakukuwa vyema akibaki nasi".
Bacca amehusishwa na klabu kama Barcelona ambao waliokua mstari wa mbele kumnasa huku Sevilla,Chelsea na Real Madrid wao wakionesha nia ya kumsajili.