Hit maker wa single ya Muziki Darassa pamoja na director Hans Cana leo hii wamepata ajali ya gari wakitokea Kahama kuelekea Geita kwa ajili ya Show na taarifa za uhakika ni kuwa wote wamenusurika kwenye ajali hiyo.
Kupitia account ya instagram darasa alituma video ikionyesha kuharibika kwa gari waliyosafiria (private car) kisha kuandika "kwenye speed 60 free road lakini icho kilichotokea miujiza lakini MUNGU ana miujiza yake pia mimi na director wangu @hanscana producer @mrvs2016 @abbah-process wote tuko poa CAN I GET AMAN FOR THAT #Muziki " aliandika darassa.
The Capital Tz.Com tunatoa pole kwa wasanii hao na kuwaombea kheri kwa kutoka salama kwenye ajali hiyo.