Chelsea ikicheza
ugenini Uwanja wa Etihad dhidi ya wenyeji Manchester City imeibuka na ushindi
wa 3-1 mbele ya vijana wa Pep Guardiola.
Gary Cahil ilijifunga
goli dakika 45, lakini kipindi cha pili dakika ya 60, Diego Costa aliifungia
Chelsea goli la kusawazisha.
Dakika ya 70, Willian
aliifungia The Blues bao la kuongoza na baadaye dakika ya 90 Eden Hazard
akachomelea msumari wa tatu kwa Chelsea.
Katika hali isiyo ya
kawaida, Sergio Aguero na Fernandinho wamezawaziwa kadi nyekundu dakika ya
mwisho.
Aguero alimchezea
madhambi mabaya David Luiz, wakati Fernandinho naye alimsukuma Fabregas mpaka
kwenye mabango ya wadhamini.