UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, Wiki hii inaingia Mechi zake za 5 za Makundi ikibakisha Mechi 1 tu na tayari Timu 5 zimeshafuzu kutinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16.
Wiki hii, Jumanne na Jumatano, Mechi hizo za 5 za Makundi zitachezwa na zipo Timu 12 ambazo zinaweza kutwaa Nafasi 11 zilizobaki huku zikibakisha Mechi 1 mkononi.
Timu ambazo haziwezi tena kusonga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 zipo 7 na hizi, pengine, zinaweza kumaliza zikiwa Nafasi za 3 za Makundi yao na hivyo kubwagwa kucheza kwenye UEFA EUROPA LIGI hatua ya Raundi ya Mtoano ya Timu 32.
+++++++++++++++++++++++++++++++
Timu 5 ambazo zimefuzu – Bado 11:
-Arsenal, Paris St Germain, Atletico Madrid, Bayern Munich, Borussia Dortmund
Timu ambazo zinaweza kufuzu Wiki hii zikibakiza Mechi 1 mkononi:
-Benfica, Napoli, Beşiktaş, Barcelona, Manchester City, Monaco, Bayer Leverkusen, Real Madrid, Leicester City, Porto, Sevilla, Juventus
Timu ambazo haziwezi kufuzu:
-Ludogorets Razgrad, Basel, PSV Eindhoven, Rostov, Brugge, Dinamo Zagreb, Legia Warszawa
+++++++++++++++++++++++++++++++
Yafuatayo ni hesabu ya Kundi kwa Kundi nafasi za Timu hizo kufuzu:
Jumanne Novemba 22
**Mechi zote kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku isipokuwa ile ya CSKA v Leverkusen ambayo itaanza Saa 2 Usiku.
KUNDI E: CSKA Moskva (Pointi 2) v Bayer Leverkusen (6), Monaco (8) v Tottenham Hotspur (4)
Monaco watafuzu wakipata Sare na watatwaa ushindi wa Kundi wakishinda wakati Leverkusen wakikosa ushindi.
Leverkusen watasonga wasipofungwa huku Tottenham wakifungwa.
CSKA lazima washinde ili wabaki Mashindanoni.
KUNDI F: Borussia Dortmund (Pointi 10, Imeshafuzu) v Legia Warszawa (1), Sporting CP (3) v Real Madrid (8)
Dortmund watakaa kileleni mwa Kundi wakishinda wakati Real Madrid wakikosa ushindi.
Real Madrid watasonga na kuitupa nje Sporting Lisbon wakitoka Sare.
KUNDI G: FC København (Pointi 5) v Porto (7), Leicester City (10) v Club Brugge (0)
Leicester watasonga kwa Sare au ikitikea FC Copenhagen hawashindi.
Porto watasonga kwa ushindi.
Brugge wanahitaji ushindi kujiweka hai huku wakiomba FC Copenhagen wang’oke kuwania Nafasi ya 3.
KUNDI H: Sevilla (Pointi 10) v Juventus (8), Dinamo Zagreb (0) v Lyon (4)
Sevilla watasonga kwa Sare na kuchukua ushindi wa Kundi kwa ushindi.
Juventus watafuzu kwa ushindi au ikiwa Lyon hawatashinda.
Lyon watamaliza Nafasi ya 3 kwa Sare wakati Dinamo wanahitaji ushindi ili kujiweka hai.
Jumatano Novemba 23
**Mechi zote kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku isipokuwa zile za Beşiktaş v Benfica (Itaanza Saa 2 Dakika 45 Usiku) na Rostov v Bayern (Saa 2 Usiku)
KUNDI A: Arsenal (Pointi 10, Imeshafuzu) v Paris Saint-Germain (10, Imeshafuzu), Ludogorets Razgrad (1) v Basel (1)
Yeyote atakaeshinda kati ya Arsenal na PSG atatwaa ushindi wa Kundi.
Yeyote atakaeshinda kati ya Ludogorets na Basel atatwaa ushindi wa 3.
KUNDI B: Beşiktaş (Pointi 6) v Benfica (7), Napoli (7) v Dynamo (1)
Ikiwa Benfica watashinda watafuzu na pia Napoli ikiwa nao watashinda.
Ikiwa Beşiktaş watashinda na Napoli hawashindi, basi Beşiktaş watasonga.
Dynamo watabaki tu kwenye kinyang’anyiro cha kufuzu ikiwa Beşiktaş hawashindi.
Dynamo watabaki Nafasi ya 4.
KUNDI C: Celtic (Pointi 2) v Barcelona (9), Borussia Mönchengladbach (4) v Manchester City (7)
Barcelona watafuzu wakishinda au wakipata Sare ikiwa Manchester City hawafungwi.
Barcelona watatwaa ushindi wa Kundi wakishinda na City kukosa ushindi.
Manchester City watafuzu wakishinda.
Mönchengladbach watwaa Nafasi ya 3 kwa Sare ikiwa Celtic watafungwa.
Ili kubaki kinyang’anyiro cha kufuzu, Celtic lazima washinde na kuombea City hawashindi.
KUNDI D: Rostov (Pointi 1) v Bayern (9, Imeshafuzu), Atlético (12, Imeshafuzu) v PSV (1)
Atlético na Bayern zimeshafuzu na Atletico watatwaa ushindi wa Kundi wakishinda wakati Bayern wanatoka Sare au kufungwa.
Mshindi wa 3 atapatikana baada ya Mechi ya mwisho.