David Alaba, beki wa Bayern Munich yupo kwenye rada za Manchester United na meneja Jose Mourinho kwa mujibu wa habari.
Nyota huyo raia wa Austria, mwenye umri wa miaka 24, bado ana mkataba Allianz Arena hadi 2021, na inasemekana anafuatiliwa na maskauti wa United tangu kipindi cha mapumziko ya kimataifa.
Inadaiwa na The Mirror kuwa Mourinho anatafuta beki matata wa kushoto na kiungo mkabaji – nafasi ambazo nyota huyo mahiri wa Bayern anazimudu.
Pamoja na kumfukuzia Alaba, habari hizo hizo zimedai kuwa mchezaji mwenzake wa Austria Julian Baumgartlinger pia yumo kwenye rada za Mashetani Wekundu - hii inamaanisha siku za Morgan Schneiderlin zinahesabika Old Trafford.
Alaba pia yupo kwenye rada za Real Madrid, wakati Baumgartlinger – ambaye ndio kwanza amjiunga na Bayer Leverkusen akitokea Mainz 05 majira ya joto – anakodolewa macho na klabu tele za barani Ulaya.