November 29 2016 Amiri Jeshi mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli amefanya ziara ya kushtukiza katika gereza la Ukonga Dar es salaam na kupiga marufuku uuzwaji wa sare za majeshi nchini na watu binafsi na kutaka wale wote wanaouza sare wazikabidhi kwa majeshi husika mara moja.
Aidha Rais Magufuli ametoa Bilioni 10 kwa jeshi la magereza kwa ajili ya kujenga nyumba mpya zitakazotumika kwa ajili ya askari wa jeshi la magereza katika gereza la Ukonga jijini DSM.
Rais Magufuli pia ameliagiza jeshi la magereza kuhakikisha wafungwa wanatumika katika uzalishaji mali badala ya mfumo wa sasa ambapo baadhi ya wafungwa wamekuwa wakitumia rasilimali za serikali bila kuzifanyia kazi.