November 29 2016 mkuu wa mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana amekutana na waandishi wa habari na kutoa ufafanuzi wa kifo cha aliyekuwa baba mzazi wa Waziri mkuu mstaaru Mizengo Pinda mzee Xavery Pinda kilichotokea mkoani hapo pamoja na ratiba ya kuaga mwili wa marehemu
‘Mzee Pinda amefariki akiwa na miaka 90, alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya viungo na kusababisha kushindwa kutembea kwa muda‘ –RC Rugimbana
‘Tatizo la mwisho lililosababisha mauti yake ni figo kushindwa kufanya kazi, juzi alipelekwa hospital baada ya kukosa fahamu‘- RC Rugimbana
‘Kesho tunatarajia kuaga mwili wa marehemu Xavery Pinda na kisha kumsafirisha kwenda mkoani Katavi kwa ajili ya mazishi‘ –RC Rugimbana
Unaweza kuendelea kumsikiliza RC Rugimbana kwenye hii sauti hapa chini…