MAMBO 15 ameyaongea Ruge Mutahaba, Tuzo, Muziki, Ruby, Lady J Dee, TID, Fiesta2017 - CAPITAL TZ BLOG DODOMA

Latest

BANNER 728X90

Friday, 25 November 2016

MAMBO 15 ameyaongea Ruge Mutahaba, Tuzo, Muziki, Ruby, Lady J Dee, TID, Fiesta2017

Leo November 25, 2016 ndani ya XXL ya Clouds FM kulikuwa na Exclusive Interview na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group (CMG) Ruge Mutahaba ambapo amezungumzia mambo kadhaa ambayo yalikuwa na maswali mengi mtaani.
Miongoni mwa vitu Ruge amevitolea ufafanuzi ni pamoja na kinachozungumzwa mitaani kwamba kuna wasanii ambao ametofautiana nao na amesimamisha nyimbo zao kuchezwa Clouds kitu ambacho Ruge amesema yeye binafsi hana tofauti na msanii yeyote isipokuwa wasanii wanaotofautiana na taasisi ya Clouds Media kinachofanyika ni kufata sheria za kampuni tu.
Pia kuna tatizo la uchache wa tuzo za wasanii Tanzania kitu ambacho amesema Baraza la Sanaa la Taifa BASATA linachangia kudidimiza hatua za sanaa kwa kuzuia wadau kuanzisha tuzo nyingine, pia utaratibu wa kufungia Video zao linatengeneza umaarufu wa wasanii na video zao badala ya kuboresha kama wanavyotaka wao.