NJOMBE.
Wakazi Wa wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe wameiomba serikali kuwasogezea karibu huduma ya kituo cha afya ili baadhi ya wanaume ambao hawajafanyiwa tohara waweze kupatiwa huduma hiyo kwani baadhi yao wamekuwa wakidai huduma zipo mbali hivyo wanashindwa kufika huko.
Ombi hilo limeombwa na baadhi ya wanaume ambao hawajafanyiwa tohara katika kijiji cha Itowo kata ya Mdandu wilayani Wanging'ombe ambao wamemweleza mhamasishaji wa eneo hilo kuwa wanashindwa kwenda kufanyiwa tohara kutokana na umbali uliopo hadi kufika katika hospitali ya Kibena Njombe ambako huduma hiyo pia inapatikana.
Akizungumza na mwandishi wa Green Fm Grace Sanga, mmoja wa waelimishaji hao amesema kuwa hivi sasa muamko wa wanaume kwenda kufanyiwa tohara umekuwa mkubwa kutoka na elimu inayoendelea kutolewa kwa wanaume kuhusu faida na hasara za kutofanya tohara.
Pia imeelezwa kuwa kumekuwa na baadhi ya changamoto mbalimbali kwa baadhi ya wanaume kama vile kuogopa kufanyiwa tohara kipindi cha msimu wa joto kwa Imani kuwa vidonda vitachelewa kupona, na wengine wakiamini kuwa baada ya kufanyiwa tohara nguvu za kiume zitapungua hivyo kuwafanya washindwe
Hivyo wanaume ambao bado hawajafanyiwa tohara wametakiwa kuachana na Imani potofu na kushauriwa kuchukua hatua ili kujikinga wao pamoja na wenza wao na maradhi yanayosababishwa na kutofanyiwa tohara.
Na Grace Sanga