Mwanafunzi wa kidato cha nne,
Flora Athanas (18) wa sekondari Mzindakaya wilayani hapa amejiua kwa
sumu ya panya, baada ya kubakwa na mtu asiyefahamika.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda, alisema jana kuwa mwanafunzi huyo alibakwa usiku wa kuamkia Jumanne yeye na mwenzake, katika chumba walimopanga, kutokana na kukosekana kwa mabweni katika shule hiyo.
Kwa mujibu wa Kamanda Mwaruanda, siku hiyo Flora alikuwa na wanafunzi wenzake watatu, akiishi nao katika chumba hicho.
Inadaiwa usiku mtu asiyefahamika, alivamia nyumba walimopanga, akafunga vyumba vya wanafunzi wengine na kuingia chumba cha akina Flora akiwa na kisu na kuwatishia kuwa atakayepiga kelele atamuua kwa kisu. READ MORE