Dar es Salaam. Rais Jakaya Kikwete ametuma
ujumbe kwa wale wanaoitishia Tanzania. Amewaambia wakithubutu watakiona
cha mtemakuni kama ilivyokuwa kwa Idd Amin wa Uganda. Alisema mamlaka za ulinzi na usalama zilimdhibiti
Amin alipofanya uvamizi katika ardhi ya Tanzania mwaka 1978 na kwamba
hazitashindwa kufanya hivyo kwa mtu mwingine yeyote atakayechezea
usalama wa nchi. Wakati Rais akisema hayo, Mkuu wa Majeshi,
Jenerali Davis Mwamunyange amewahakikishia wananchi kuwa wakati wote
jeshi liko imara na kuwataka wasiogope lolote. Viongozi hao walisema hayo jana katika maadhimisho
ya Siku ya Mashujaa iliyofanyika katika Kambi ya Jeshi ya Kaboya
iliyopo Muleba, Kagera. “Sihitaji kusema tena, mmeshamsikia Mkuu wa
Majeshi, atakayejaribu atakiona cha mtemakuni, laleni usingizi na msiwe
na wasiwasi, msisikilize maneno ya mitaani,” alisema Rais Kikwete na
kuongeza: READ MORE
Friday, 26 July 2013
New
About Unknown
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
