HUYU NDIYE MWALIMU ALIYETELEKEZA WANAFUNZI NA KUWA ‘MC’ - CAPITAL TZ BLOG DODOMA

Latest

BANNER 728X90

Sunday, 7 July 2013

HUYU NDIYE MWALIMU ALIYETELEKEZA WANAFUNZI NA KUWA ‘MC’

Kwa tafasiri ya haraka inaweza kuwashangaza watu wengi na kuhoji nini kulikoni kwa mtumishi wa umma tena mwenye taaluma ya kufundisha kwa ngazi ya elimu ya sekondari, kufikia hatua ya kuacha taaluma hiyo na kuingia kwenye ajira binafsi ya ushereheshaji wa hadhira(MC). Lakini moja kati ya changamoto kubwa zinazoikabili Serikali katika sekta ya elimu ni kilio cha walimu kupata mishahara kidogo, kukosa makazi ya kuishi na vitendea kazi, mchango kidogo kwa Serikali na mtazamo hasi uliopo katika jamii. 
Mambo hayo yanaweza kuwa sababu ya mwalimu Emmanuel Mathias (28), kutoka shule ya sekondari ya DCT Jubilee iliyopo mkoani Dodoma, ambaye ameacha ualimu na kuwa kati ya ma- MC maarufu hapa nchini. Hakupata wakati mgumu na haoni sababu ya kujutia kabisa uamuzi huo baada ya kuacha taaluma hiyo kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita. Alifahamika kwa jina la mwalimu Emmanuel lakini kwa sasa ni MC Pilipili......READ MORE