New
Katika
orodha hii nafasi ya kwanza kabisa anashikilia mwanamama Oprah, na hii
ni kutokana na nguvu yake kubwa katika Televisheni pamoja na mitandao ya
kijamii, na pia anamiliki wa Cable Network kubwa kabisa ya Oprah, na
kwenye rekodi inaonyesha kuwa kati ya mwezi June 2012 na June 2013
amejivunia kiasi cha dola milioni 77, sawa na shilingi 124,008,500,000
za kitanzania .
Katika
nafasi ya pili anasimama, Lady Gaga ambaye ana nyota ya kupendwa na
watu kutoka kona zote za dunia, akiwa anaongoza kufuatwa katika social
networks hasa kutokana na muonekano wake wa kitofauti zaidi na Uwezo
kimuziki, licha ya kuwa nnje ya stage kwa muda akiwa anapona uparesheni
ya hips, ameweza kujivunia dola milioni 80, sawa na pesa za kitanzania,
shilingi 128,840,000,000 katika kipindi cha mwaka jana mpaka mwaka huu.
Katika
nafasi ya tatu anasimama TV/Film Director/Producer maarufu Steven
Spielberg ambaye yupo nafasi ya juu kabisa na anaheshimika katika fani
hiyo akiwa ni mtu mzima mwenye umri wa miaka 59, Huyu kwa mwaka
amejitengenezea dola milioni 100, sawa na shilingi 161,050,000,000 za
kitanzania.
Katika
nafasi inayofuata anasiamama mwanadada Beyonce ambaye mafanikio yake
yanafahamika kote, akiwa amejivunia dola milioni 53, sawa na shilingi
85,356,500,000 za kitanzania.
Pia
kuna mkongwe Madonna katika nafasi ya tano, akiwa ametengeneza dola
milioni 125, sawa na shilingi 201,312,500,000 za kitanzania.
Nafasi ya sina inashikiliwa na Taylor Swift, dola milioni 55, sawa na shilingi za kibongo 88,577,500,000.
Nafasi inayofuata inakamatwa na Jon Bon Jovi, dola 79, sawa na shilingi za bongo 127,229,500,000.
Nafasi
ya saba inashikiliwa na mwanamichezo wa Tennis, Roger Federer ambaye
anashikilia dili nono na makampuni makubwa mbalimbali hasa yale
yanayofanya biashara ya vifaa vya michezo, dola milioni 71, pesa za
madafu 114,345,500,000.
Nafasi
inayofuata inashikiliwa na mwanamuziki kinda, Justin Bieber, dola
milioni 85, zinazolingana na pesa za kibongo 93,409,000,000.
Na katika nafasi ya 10 yupo mtangazaji mkali kabisa wa TV, Ellen DeGeneres, huyu akiwa na dola milioni 83 ndani ya mwaka mmoja, sawa na shilingi 85,356,500,000 za Tanzania.
#Vigezo
vya Forbes katika orodha hii vimezingatia mapato waliyoingiza wasanii
hawa kutoka mwezi Juni mwaka jana mpaka mwaka huu, na pia namba ya watu
ambao wanawatazama na kuwafuatilia kwa karibu.