SIO BONGO TU!! VILLA YA UGANDA YASAJILI MCHEZAJI WA LIGI DARAJA LA TATU KUTOKA IVORY COAST... - CAPITAL TZ BLOG DODOMA

Latest

BANNER 728X90

Monday, 26 September 2016

SIO BONGO TU!! VILLA YA UGANDA YASAJILI MCHEZAJI WA LIGI DARAJA LA TATU KUTOKA IVORY COAST...



 
Chini ya mwezi mmoja baada ya kumsajili  Mbrazil Tiago Franc Lino Alves na Mburundi Fuadi Ndayisenga, SC Villa "Jogoo"  imesaini nyota mwingine mgeni, Boue Bi Marc Olivier aliyekuwa anacheza klabu ya Atlantis FC inayoshiriki Ligi daraja la Tatu.



Mshambuliaji huyo wa Ivory Coast amesaini  mkataba wa miaka miwili na  Villa ambapo Raisi wa klabu hiyo  Ben Immanuel Misagga alimtangaza mbele ya wanahabari mchezaji huyo.



"Nina furaha bado kutangaza mshambuliaji mwingine mpya kutoka Ivory Coast,  Lengo letu ni kushinda Ligi Kuu msimu huu na tunaweza tu kushinda kwa kufunga mabao. Sisi tumemkubali  ni mtu bora kwetu alikuwa anacheza Atlantis kutoka Kwao  ambapo yeye anadai kuwa amefunga mabao 10 msimu uliopita kwahiyo ni mchezaji mzuri sana.



Boue Bi anatarajiwa kucheza mechi yake ya kwanza kesho Jumanne nyumbani kwa Soana Fc  ambao wamefungwa mabao matatu tu baada ya mechi sita.