Jumapili ya octoba 2 klabu ya mtibwa suger itashuka uwanjani kwao Manungu Complex kuivaa African Lyon katika mchezo wa ligi kuu Vpl Tanzania Bara na ni mojawapo ya timu iliyoandamwa na nyota wake kuwa na majeraha.
Hii hapa Report kutoka kwa daktari wa timu hiyo
SALIM MBONDE
Beki huyo wa katikati aliumia katika mchezo dhidi ya Mbao na kushindwa kuendelea na mchezo .
report ya daktari inaonesha Salim Mbonde anasumbuliwa na nyama za paja.
KELVIN FRIDAY KELUU
Kelvin Friday anayemudu kiungo mshambuliaji akitokea pembeni yeye anaendelea na matibabu na anaendelea vizuri na report ya daktari inaonesha Winger huyo anasumbuliwa na kifundo cha mguuu
SAID NDUDA
Said Nduda ambaye ni golikipa wa kutumainiwa wa Mtibwa Sugar kwa misimu kwa sasa yeye anasumbuliwa na goti ila kwa mujibu wa daktari wa timu Said anakaribia kuanza mazoezi mepesi mepesi ili kujiweka fiti.
Kwa mujibu wa daktari wachezaji watatu tu ndo wana serious injury ila Said Nduda anaelekea katika kuanza mazoezi na wenzake karibuni.
Kama ulipitwa, Tazama hapa chini Video ya magoli Mechi ya Mtibwa Fc Vs Mbao Fc