SMALLING AMTUKUZA WAYNE ROONEY, AMUITA MTU MKUU NDANI YA UNITED.... - CAPITAL TZ BLOG DODOMA

Latest

BANNER 728X90

Monday, 26 September 2016

SMALLING AMTUKUZA WAYNE ROONEY, AMUITA MTU MKUU NDANI YA UNITED....

 Image result for chris smalling action and rooney
Chris Smalling amemsapoti Wayne Rooney na kutamka huyo ndie 'Mtu Mkuu' kwa Manchester United na England.
 
Kauli hii imekuja baada ya Jumamosi Rooney kupigwa Benchi na Meneja Jose Mourinho kwenye Mechi ya EPL, Ligi Kuu England, dhidi ya Mabingwa wa England Leicester City ambayo Man United walishinda 4-1 huku Bao zao zote zikifungwa Kipindi cha Kwanza.
 
Kuhusu kumtema Rooney, Mourinho alitoboa uchezaji wake umeathiriwa na kupondwa mno wakati akiichezea England ambayo yeye pia ndie Kepteni kama alivyo kwa Man United.
 
Mara baada ya Mechi hiyo na Leicester, Mourinho alipasua kuwa Wayne Rooney bado ni Mchezaji mkubwa kwa Timu yao.
 
Mourinho alisema ana imani yote kwa Rooney na kuwa bado ni Mchezaji muhimu kwa Timu yao licha ya kumuanzisha Benchi.
 
Hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Rooney kutoanza Mechi chini ya Mourinho na mara ya mwisho kwa Kepteni huyo kupigwa Benchi ni Desemba 26 Mwaka Jana.
 
Mourinho alieleza: "Ni Mtu wangu, namuamini kwa kila kitu. Yeye ana furaha kama mimi  na hii ndiyo Timu."
Aliongeza: "Yeye ni Mchezaji mkubwa kwangu mimi, United na ni Mchezaji mkubwa kwa Nchi hii!"