
Klabu ya soka ya Azam Fc ipo katika maandalizi kuelekea kwenye mchezo dhidi ya Simba Sc utakaopigwa wikiendi hii katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
Awali kulikuwa na taarifa kuwa mchezo huo umesogezwa mbele hivyo kuharibu ratiba ya ligi kuu vodacom Tanzania bara lakini baada ya shirikisho la soka nchini Tff kupuuza taarifa hizo mbele ya vyomo vya habari kupitia kwa ofisa habari wake Alfred Lucas timu hiyo imetamba kufanya vyema katika mchezo huo

Aidha mchezo huo unatajwa kuwa wa ushindani baada ya timu hiyo kufungana karibia kila kitu katika msimamo wa ligi.