POGBA APATA MTETEZI, WENYE MANENO YA KUBEZA WAAMBIWA ITABIDI WAYAMEZE!! - CAPITAL TZ BLOG DODOMA

Latest

BANNER 728X90

Tuesday, 13 September 2016

POGBA APATA MTETEZI, WENYE MANENO YA KUBEZA WAAMBIWA ITABIDI WAYAMEZE!!

Image result for POGBA WITH ZLATAN ACTION
Mshambuliaji mahiri wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic Al maarufu Kama “Ibracadabra” amemtetea mchezaji mwenzake Paul Pogba kutokana na kushindwa kuonyesha kiwango cha juu zaidi katika mechi zake za kwanza za Ligi Kuu nchini Uingereza msimu huu.

Zlatan ambaye amepachika mabao manne mpaka sasa amesema wale wote wanao uliza maswali juu ya dau lake kubwa la uhamisho watalazimishwa kuyameza maneno yao.

“Wale wote wenye wivu wanao muongelea, watakuja kumeza maneno yao yote” alisema Zlatan
Kiungo huyo kutoka Ufaransa mwenye umri wa miaka 23 amecheza mechi tatu za ligi juu nchini Uingereza na hajaandika bao wala pasi pasi yoyote ya mabao.

“Pogba ataimarika zaidi na atapewa sapoti ya kila mtu. Uhusiano wangu na yeye ni mrahisi. Mimi ninaongea yeye anasikiliza. Paul ni mchezaji mwenye vipaji vingi mno” aliongeza

“Kiukweli watu wanamuwekea presha kubwa, usajili wake ulizalisha maneno mengi sana. Sikuwahi kumfahamu Pogba Ila ni mtu ambaye anajituma sana na atakuja kuwa bora sana”