UEFA CHAMPIONS LEAGUE KILINGENI LEO, UPO HAPA UCHAMBUZI WA MECHI KUBWA NA RATIBA KAMILI... - CAPITAL TZ BLOG DODOMA

Latest

BANNER 728X90

Tuesday, 13 September 2016

UEFA CHAMPIONS LEAGUE KILINGENI LEO, UPO HAPA UCHAMBUZI WA MECHI KUBWA NA RATIBA KAMILI...

 Image result for Laurent Koscielny action
PSG vs Arsenal | Jumanne Septemba 13, 2016 | Parc des Prices Ufaransa

Arsenal wamepata nguvu ya kujiamini baada ya Laurent Koscielny kufanya mazoezi na kikosi cha klabu hiyo kuelekea mechi ya kwanza Ligi ya Mabingwa dhidi ya Paris Saint Germain katika uwanja wa Parc des Princes Jumanne.

Beki huyo wa kati alipata majeraha Arsenal iliposhinda 2-1 dhidi ya Southampton, ambapo alipiga bao safi la mkasi, lakini alifanya mazoezi mjini London Jumatatu.

Arsene Wenger, ambaye aliweza kupumzisha wachezaji kadhaa katika ushindi wa Jumamosi, anataraji wakuchezesha kikosi thabiti katika jiji kuu la Ufaransa leo usiku.

Mchezaji mpya Shkodran Mustafi anaweza kucheza pamoja na Koscielny, Arsenal ikiwa inaikosa huduma ya Per Mertesacker na Gabriel ambao wote ni majeruhi.

Habari za Timu
Wenger amethibitisha kuwa Koscielny yupo njema na atacheza, lakini Aaron Ramsey bado hajawa tayari kucheza mechi hiyo licha ya kuanza mazoezi Jumatatu.

Olivier Giroud naye anataka kuanza kikosi cha kwanza kwa mara ya kwanza baada ya kuanzia benchi katika mechi mbili alizocheza msimu huu.

Takwimu
Paris Saint-Germain mara ya mwisho walikutana na Arsenal 1993/94 nusu fainali ambapo Gunners walishinda kwa jumla ya magoli 2-1.

Arsenal hawajawahi kufungwa katika mechi zao 12 za ugenini dhidi ya klabu za Ufaransa kwenye michuano ya Ulaya, ikiwa ni pamoja na mechi zao saba za mwisho.

Barcelona vs Celtic | Jumanne Septemba 13, 2016 | Camp Nou, Barcelona
 Image result for scott brown action
Nahodha wa Celtic Scott Brown yupo fiti kuikabili Barcelona Ligi ya Mabingwa katika hatua ya makundi mechi ya ufunguzi itakayopigwa kwenye uwanja wa Nou Camp Jumanne

Meneja msaidizi Chris Davies amesema mabingwa hao wa Uskochi wamedhamiria kuishikisha adabu Barcelona ambayo ilichezea kichapo cha 2-1 kutoka kwa Alves iliyopanda daraja.

Luis Enrique kwa upande wake anatarajia kikosi chake kijibu kichapo cha La Liga kwa kuifunga Celtic mechi hiyo ya kwanza.

Enrique mambo yalimwendea kinyume baada ya kufanya mabadiliko saba - ikiwa ni pamoja na kuwaacha benchi Lionel Messi,na Luis Suarez mwanzo wao wa ushindi kwa asilimia 100 ulipokoma mikononi mwa Alves iliyopata ushindi wa kwanza Barcelona ndani ya muongo mmoja.

Habari za Timu
Kinara wa mabao wa Celtic Leigh Griffiths atakosa mchezo huu kutokana na majeraha ya misuli, Moussa Dembele atachukua nafasi yake.

Messi, Suarez na Andres Iniesta wanatarajiwa kuanza kukosi cha kwanza Barcelona baada ya kupumzishwa Jumamosi.

Kipa Jasper Cillessn alianza kuichezea Barca kwa mara ya kwanza Jumamosi na Marc-Andre ter Stegen, ambaye anaweza kurejea mapema kuliko inavyotarajiwa alianza mazoezi Jumatatu.

Takwimu 
 Barcelona imeshinda mechi sita kati ya nane za Ligi ya Mabingwa dhidi ya Celtic, ambapo ushindi wa Celtic ulipatikana Novemba 2012 walipoifunga Barcelona 2-1 katika uwanja wa Celtic Park.

Celtic imepoteza mechi tatu katika uwanja wa Nou Camp, zote zikiwa ni Ligi ya Mabingwa.
Messi ametupia mabao 83 katika Ligi ya Mabingwa, idadi kubwa ya magoli akishika nafasi ya pili nyuma ya Cristiano Ronaldo 93.

Hat-trik ya kwanza ya Neymar kwa Barcelona imepatikana dhidi ya Celtic katika Ligi ya Mabingwa Desemba 2013, Barcelona walipoiadhibu klabu hiyo ya Uskochi bao 6-1.

 Manchester City vs Borussia Monchengladbach | J'nne Sept 13, 2016 | Etihad
 Image result for sergio aguero action


Sergio Aguero yupo tayari kuikabili Borussia Monchengladbach katika mechi hiyo ya Manchester City Ligi ya Mabingwa hatua ya makundi itakayopigwa kwenye uwanja wa Etihad Jumanne.

Mwargentina huyo alikosa mechi ambayo timu yake ilitoka kifua mbele dhidi ya Manchester United kwa kufungiwa na Shirikisho la Uingereza, lakini Pep amethibitisha kuwa mshambuliaji huyo wa City anaweza kucheza dhidi ya klabu hiyo ya Bundesliga.

City wanatarajia kuutumia vema uwanja wao wa nyumbani dhidi ya timu waliyoifunga mara mbili msimu uliopita.

Guardiola ambaye alibainisha kuwa Ilkay Gundogan na Vincent Kompany wanakaribia kurudi kikosi cha kwanza alisema: "Aguero anaweza kucheza - alifungiwa tu mechi wala si majeruhi.
 Image result for pep guardiola action

UEFA CHAMPIONZ LIGI RATIBA KAMILI
*Mechi zote kuanza Saa 3 Dakika 45 Usiku, Bongo Taimu
Jumanne 13 Septemba 2016
KUNDI A
Basel v Ludo Razgrad                 
Paris St Germain v Arsenal                  
KUNDI B
Benfica v Besiktas            
Dynamo Kiev v Napoli                
KUNDI C
Barcelona v Celtic             
Man City v Borussia Monchengladbach             
KUNDI D
Bayern Munich v FC Rostov                   
PSV Eindhoven v Atletico Madrid