Mwishoni mwa wiki iliyopita Ngassa alivunja mkataba
wa kuichezea Free State kwa madaia timu hiyo haina malengo ya kushinda
mataji kwenye ligi ya ABSA
Kocha wa Mbeya City Kinnah Phiri, amesema yupo tayari kumsajili winga Mrisho Ngassa endapo timu yake ya zamani Yanga itashindwa kufanya hivyo.
Phiri amesema, amekuwa shabiki mkubwa wa mchezaji huyo na ndio sababu ya kumsajili Free State kabla hajafukuzwa msimu uliopita.
"Nitaongea na viongozi wangu kuna kama tunaweza kumuongeza Ngassa kwenye dirisha dogo lakini hiyo itatokana na utayari wake wa kutaka kucheza kwetu maana nasikia anamapenzi mkubwa na Yanga," amesema Phiri.
Mwishoni mwa wiki iliyopita Ngassa alivunja mkataba wa kuichezea Free State kwa madaia timu hiyo haina malengo ya kushinda mataji kwenye ligi ya ABSA.