BAADA YA KUITUNGUA STARS, IHENACHO AJAZWA SIFA NA CHELSEA - CAPITAL TZ BLOG DODOMA

Latest

BANNER 728X90

Sunday, 4 September 2016

BAADA YA KUITUNGUA STARS, IHENACHO AJAZWA SIFA NA CHELSEA

 Image result for KELECHI IHEANACHO ACTION
Chelsea ilivutiwa na pambano la Nigeria dhidi ya Tanzania kwa sababu ya Obi Mikel na Victor Mosses lakini bao la Iheanacho liliwavutia zaidi

Katika uchambuzi wa mechi ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika baina ya Nigeria na Tanzania, tovuti rasmi ya Chelsea ilimsifia mshambuliaji wa Manchester City Kelechi Iheanacho baada ya kufunga goli pekee lililoipa ushindi murua Super Eagle.

Blues walivutiwa na pambano hilo katika uwanja wa Akwa Ibom International kwa sababu ya wachezaji wawili muhimu sana kwao, John Obi Mikel na Victor Moses ambao walikuwame dimbani.

"Super Eagles walikuwa wanafahamu kwamba hawatafuzu kwa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Januari baada ya kushindwa kung'ara kwenye kampeni za kufuzu, lakini walimaliza kwa ushindi dhidi ya wapinzani wao wa Afrika Mashariki kwa bao safi kutoka kwa Kelechi Iheanacho dakika 12 kabla ya kipyenga cha mwisho kupulizwa.

"Mikel alicheza dakika 81 akipata nafasi nzuri mara kadhaa," Chelsea ilisema kupitia tovuti yao