NYOTA WA ZAMANI YANGA AANZA TAMBO, ADAI WAJIANDAE KWA KIPIGO.. - CAPITAL TZ BLOG DODOMA

Latest

BANNER 728X90

Monday, 5 September 2016

NYOTA WA ZAMANI YANGA AANZA TAMBO, ADAI WAJIANDAE KWA KIPIGO..

 Image result for kigi makasi kigi
Nahodha wa Ndanda FC Kigi Makasi ameitahadharisha Yanga kujiandaa na kipigo kwani hawapo tayari kupoteza mechi tatu mfulizo

Makasi mchezaji aliyepata jina akiwa na Yanda ameiambia Goal, wamejipanga kuhakikisha hawapati tena matokeo mabaya kwenye mchezo huo ambao ameuita ni sawa na fainali kwao.

"Tunajua tumeshapoteza mechi za kwanza tayari, na Yanga ni mabingwa watetezi ambao kwa hakika wapo vizuri sana, lakini tumedhamiria na tutahakikisha tunachukua pointi zote tatu," amesema Makasi.

Yanga itasafiri hadi Mtwara tarehe saba mwezi huu kuifuata Ndanda itakayocheza kwenye uwanja wa nyumbani Nangwanda Sijaona Mtwara saa 10 jioni.