MWANAMKE MKAZI WA MLIMWA, DODOMA, FATUMA MOHAMED, ANASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMUUA MTOTO WA MKE MWENZAKE, - CAPITAL TZ BLOG DODOMA

Latest

BANNER 728X90

Friday, 22 April 2016

MWANAMKE MKAZI WA MLIMWA, DODOMA, FATUMA MOHAMED, ANASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMUUA MTOTO WA MKE MWENZAKE,


Mwanamke mkazi wa Mlimwa, Dodoma, Fatuma Mohamed, anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumuua mtoto wa mke mwenzake, kisha kutumbukiza mwili wake kwenye karo la maji. Mtoto aliyeuawa, Subira Ganyara mwenye umri wa mwaka mmoja, aliibwa Aprili 19 nyumbani kwa mama yake Agnes Yohana saa 3 usiku wakati akiwa amelala chumbani. Mtoto huyo alipatikana Aprili 20, akiwa amenyongwa na kutumbukizwa kwenye karo la maji lililokuwa wazi.