HUU NDIO MWAKA AMBAO SERIKALI ITAANZA KUTOA MILIONI 50 KILA KIJIJI. - CAPITAL TZ BLOG DODOMA

Latest

BANNER 728X90

Friday, 22 April 2016

HUU NDIO MWAKA AMBAO SERIKALI ITAANZA KUTOA MILIONI 50 KILA KIJIJI.

Serikali imesema itaanza kutekeleza ahadi ya Rais John Magufuli ya kukipa kila kijiji nchini Sh milioni 50  katika mwaka wa fedha wa 2016-2017.
Kauli hiyo ilitolewa bungeni jana na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Sera, Uratibu, Bunge la Walemavu, Antony Mavunde alipojibu swali la  Mbunge wa Viti Maalumu, Halima Bulembo.
Bulembo alitaka kujua   ahadi ya Sh milioni 50 kwa kila kijiji itatekelezwa lini.
Mavunde alisema ahadi ya Rais Magufuli ya kila kijiji kupewa Sh milioni 50 itaanza kutekelezwa  katika mwaka wa fedha wa 2016-2017.
Alisema utaratibu wa kugawa fedha hizo unaandaliwa na Baraza la Uwezeshaji Wananchi kwa kushirikiana na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.
‘’Pamoja na mikakati yote hiyo vigezo ambavyo vimekuwa vikitumika katika kutoa mikopo  na mitaji  kwa vijana ni umri usiozidi miaka 35 ambavyo  ni kujiunga na Saccos za vijana za wilaya na kuunda vikundi na kuvisajili kisheria,” alisema.
Alisema ili kuhakikisha vijana wanakuwa wajasiriamali na wanaweza kupatiwa mikopo na mitaji, serikali imejiwekea mikakati ya kutambua vijana na mahitji yao katika ngazi mbalimbali  na kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa makundi mbalimbali ya vijana.